Soma Biblia Kila Siku 04/2025Mfano

Kuhani aliwaleta watu karibu na Mungu kwa njia ya matoleo ya sadaka kwa ajili ya dhambi. Alikuwa pia na wajibu wa kufundisha watu Neno la Mungu.Watamfundisha Yakobo hukumu zako, Na Israeli torati yako(Kum 33:10; “hukumu” na “torati” humaanisha yote Neno la Mungu). Sasa Haruni na wanawe wanawekwa wakfu, ili kazi hizi za kupatanisha watu na Mungu na kutoa mafundisho zifanyike. Ilibidi watakaswe kwanza, tofauti na Yesu, Kuhani Mkuu wa agano jipya, ambaye ni mkamilifu bila waa lolote. Amechukua nafasi ya yule kuhani wa Agano la Kale na kutuletea wokovu mkuu.Ilimpasa[Yesu]kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake(Ebr 2:17). Zingatia swali katika Ebr 2:3:Sisi je, tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii?
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 04/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Aprili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Walawi, Luka na 2 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz