Soma Biblia Kila Siku 09/2025Mfano

Watu wanaokutana na Bwana Yesu katika Injili wanabadilika, maana Roho Mtakatifu anafanya kazi kupitia neno hilo.Sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho(3:18).Kwa sababu hiyo(m.1) Paulo hakati tamaa. Kupotosha na kupindisha Neno la Mungu huja kwa njia ya kujipendekeza au kuwaridhisha wasikilizaji. Lakini kama Paulo, sisi nasi tumeitwa kumshuhudiaYesu Kristotukitangazakweliya Neno la Mungu na si vinginevyo. Njia yetu ni daima kuidhihirisha kweli waziwazi tukiilenga kwa dhamiri za watu. Hivyo nuru itang’aa mioyoni mwao.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 09/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Septemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 1 Nyakati na 2 Wakorintho. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz
