Soma Biblia Kila Siku 09/2025Mfano

Mungu hatutumii sisi kama vyombo vyake ili kuonesha thamani yetu. Sisi tu vyombo vya udongo, lakini Mungu akiishi na kutenda kazi ndani yetu, anaweza kuonesha wokovu usioharibika, na kwamba umetoka kwake wala si kutoka kwetu. Hivyo tuna thamani kubwa na isiyopimika mbele ya Mungu. Ingawa tunaonekana dhaifu, Mungu ametupa uwakili wa Neno lake. Wajibu wetu ni kuwa kama Kristo kwa wengine ili wamwone Yesu kupitia kwetu. Tafakari jinsi utakavyoweza kumshuhudia Yesu namna hiyo, ukikumbuka Yesu mwenyewe anavyoeleza:Awapokeaye ninyi, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi, ampokea yeye aliyenituma(Mt 10:40).
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 09/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Septemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 1 Nyakati na 2 Wakorintho. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz
