1
Kumbukumbu 28:1
Neno: Bibilia Takatifu
Kama ukimtii BWANA Mungu wako kwa bidii na kufuata amri zake zote ninazokupa leo kwa bidii, BWANA Mungu wako atakuweka juu ya mataifa yote katika dunia.
Linganisha
Chunguza Kumbukumbu 28:1
2
Kumbukumbu 28:2
Baraka hizi zote zitakuja juu yako na kukupata, kama ukimtii BWANA Mungu wako
Chunguza Kumbukumbu 28:2
3
Kumbukumbu 28:13
BWANA atakufanya kichwa, wala si mkia. Kama utazingatia maagizo ya BWANA Mungu wako ninayokupa siku hii ya leo na kuyafuata kwa bidii, daima utakuwa juu, kamwe hutakuwa chini.
Chunguza Kumbukumbu 28:13
4
Kumbukumbu 28:12
BWANA atafungua mbingu, ghala zake za baraka, kukupa mvua kwa majira yake na kubariki kazi zako zote za mikono yako. Utakopesha mataifa mengi lakini hutakopa kwa yeyote.
Chunguza Kumbukumbu 28:12
5
Kumbukumbu 28:7
BWANA atasababisha adui wainukao dhidi yako kushindwa mbele yako. Watakujia kwa njia moja lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba.
Chunguza Kumbukumbu 28:7
6
Kumbukumbu 28:8
BWANA ataagiza baraka juu ya ghala zako na juu ya kila kitu utakachogusa kwa mkono wako. BWANA Mungu wako atakubariki katika nchi anayokupa.
Chunguza Kumbukumbu 28:8
7
Kumbukumbu 28:6
Utabarikiwa uingiapo na utabarikiwa utokapo.
Chunguza Kumbukumbu 28:6
8
Kumbukumbu 28:3
Utabarikiwa mjini na utabarikiwa mashambani.
Chunguza Kumbukumbu 28:3
9
Kumbukumbu 28:4
Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na mazao ya nchi yako na wanyama wako wachanga wa kufugwa, yaani ndama wa makundi yako ya ngʼombe, na wana-kondoo wa makundi yako.
Chunguza Kumbukumbu 28:4
10
Kumbukumbu 28:9
BWANA atakufanya kuwa taifa lake takatifu, kama alivyokuahidi kwa kiapo, kama ukishika maagizo ya BWANA Mungu wako na kwenda katika njia zake.
Chunguza Kumbukumbu 28:9
11
Kumbukumbu 28:5
Kapu lako na vyombo vyako vya kukandia vitabarikiwa.
Chunguza Kumbukumbu 28:5
12
Kumbukumbu 28:11
BWANA atakupa kustawi kwa wingi, katika tunda la uzao wa tumbo lako, katika wanyama wachanga wa mifugo yako na katika mazao ya ardhi yako, katika nchi aliyowaapia baba zako kuwapa.
Chunguza Kumbukumbu 28:11
13
Kumbukumbu 28:10
Kisha mataifa yote ya dunia wataona kuwa unaitwa kwa jina la BWANA, nao watakuogopa.
Chunguza Kumbukumbu 28:10
14
Kumbukumbu 28:14
Usihalifu amri zangu zozote ninazokupa leo, kwa kwenda kuume au kushoto, kwa kufuata miungu mingine na kuitumikia.
Chunguza Kumbukumbu 28:14
15
Kumbukumbu 28:15
Hata hivyo, kama hutamtii BWANA Mungu wako na kuzishika kwa bidii amri zake zote na maagizo ninayokupa leo, laana hizi zote zitakuja juu yako na kukupata
Chunguza Kumbukumbu 28:15
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video