1
1 Mose 17:1
Swahili Roehl Bible 1937
Aburamu alipokuwa mwenye miaka 99, Bwana akamtokea Aburamu, akamwambia: Mimi ni Mungu Mwenyezi, uendelee machoni pangu na kunicha!
Linganisha
Chunguza 1 Mose 17:1
2
1 Mose 17:5
Kwa hiyo usiitwe tena jina lako Aburamu (Baba mtukufu), ila jina lako liwe Aburahamu (Baba yao wengi)! Kwani nimekuweka kuwa baba yao mataifa mengi ya watu.
Chunguza 1 Mose 17:5
3
1 Mose 17:7
Nitalisimamisha agano langu, tuliloliagana mimi na wewe nao wa uzao wako wajao nyuma yako, liwe agano la vizazi vya kale na kale, niwe Mungu wako na Mungu wao wa uzao wako wajao nyuma yako.
Chunguza 1 Mose 17:7
4
1 Mose 17:4
Tazama! Nina agano na wewe, uwe baba yao mataifa mazima ya watu.
Chunguza 1 Mose 17:4
5
1 Mose 17:19
Ndipo, Mungu aliposema: Ni kweli, mkeo Sara atakuzalia mtoto mume, nalo jina lake uliite Isaka (Acheka); naye ndiye, nitakayemsimamishia Agano langu kuwa la kale na kale kwao wa uzao wake wajao nyuma yake.
Chunguza 1 Mose 17:19
6
1 Mose 17:8
Nitakupa wewe nao wa uzao wako wajao nyuma yako nchi hii, unayoikaa ugeni, ndiyo nchi yote ya Kanaani, mwichukue, iwe yenu kale na kale, nami nitakuwa Mungu wao.
Chunguza 1 Mose 17:8
7
1 Mose 17:17
Ndipo, Aburahamu alipomwangukia usoni pake, akacheka na kusema moyoni mwake: Itawezekanaje, mwenye miaka mia azaliwe mtoto? Huyu Sara aliye mwenye miaka 90 atazaaje?
Chunguza 1 Mose 17:17
8
1 Mose 17:15
Kisha Mungu akamwambia Aburahamu: Mkeo Sarai asiitwe tena jina lake Sarai, ila jina lake liwe Sara (Mama mkuu)!
Chunguza 1 Mose 17:15
9
1 Mose 17:11
Mkizikata nyama za magovi yenu, hii itakuwa kielekezo cha Agano, tuliloliagana mimi nanyi.
Chunguza 1 Mose 17:11
10
1 Mose 17:21
Lakini lile Agano langu nitamsimamishia Isaka, Sara atakayekuzalia siku zizi hizi za mwaka ujao.
Chunguza 1 Mose 17:21
11
1 Mose 17:12-13
Kwenu kila mtoto wa kiume aliye wa vizazi vyenu akimaliza siku nane sharti atahiriwe. Vivyo hivyo nao wazalia wa nyumbani nao wasio wa uzao wako walionunuliwa kwa fedha kwa wageni wo wote. Hao wazaliwa nyumbani mwako nao walionunuliwa kwa fedha zako sharti nao watahiriwe. Hili Agano langu la kuzikata hizo nyama za miili yenu sharti liwe la kale na kale.
Chunguza 1 Mose 17:12-13
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video