1
1 Wafalme 3:9
Biblia Habari Njema
Kwa hiyo, nakuomba unipe mimi mtumishi wako moyo wa kusikia ili kuamua watu wako, niweze kutambua mema na mabaya; maana ni nani awezaye kuhukumu watu wako walio wengi hivi?”
Linganisha
Chunguza 1 Wafalme 3:9
2
1 Wafalme 3:12
basi, sasa nakutimizia kama ulivyoomba. Tazama, nakupa hekima na akili kiasi ambacho hapana mtu mwingine aliyepata kuwa nacho kabla yako, na wala hatatokea mwingine kama wewe baada yako.
Chunguza 1 Wafalme 3:12
3
1 Wafalme 3:11
naye akamwambia, “Kwa kuwa umetoa ombi hili, na hukujiombea maisha marefu au mali, na wala hukuomba adui zako waangamizwe, bali umejiombea utambuzi wa kutoa hukumu au kutenda haki
Chunguza 1 Wafalme 3:11
4
1 Wafalme 3:13
Pia, nitakupa yale ambayo hukuomba: Nitakupa utajiri na heshima zaidi ya mfalme mwingine yeyote wa nyakati zako.
Chunguza 1 Wafalme 3:13
5
1 Wafalme 3:14
Tena kama ukifuata njia na maagizo yangu na kushika amri zangu kama alivyofanya baba yako Daudi, basi, nitakupa maisha marefu.”
Chunguza 1 Wafalme 3:14
6
1 Wafalme 3:5
Huko Gibeoni, Mwenyezi-Mungu alimtokea Solomoni katika ndoto usiku, akamwambia, “Omba chochote nami nitakupa.”
Chunguza 1 Wafalme 3:5
7
1 Wafalme 3:7
Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, umeniweka mimi mtumishi wako kuwa mfalme mahali pa baba yangu Daudi, ijapokuwa ningali mtoto mdogo na sijui namna ya kutekeleza wajibu huu.
Chunguza 1 Wafalme 3:7
8
1 Wafalme 3:10
Ombi hili la Solomoni lilimfurahisha Mwenyezi-Mungu
Chunguza 1 Wafalme 3:10
9
1 Wafalme 3:6
Solomoni akamwambia, “Ulimwonesha mtumishi wako Daudi, baba yangu, fadhili nyingi, kwa sababu alikutumikia kwa uaminifu, uadilifu na kwa haki; na umedumisha fadhili zako kwa kumpa mwana anayeketi sasa kwenye kiti chake cha enzi.
Chunguza 1 Wafalme 3:6
10
1 Wafalme 3:8
Na hapa umeniweka kati ya watu wako ambao umewachagua; nao ni wengi hata hawawezi kuhesabika kwa wingi wao.
Chunguza 1 Wafalme 3:8
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video