Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021Mfano
Baraza la Wayahudi halikuwa na mamlaka ya kumhukumia Yesu kifo. Ilibidi wamwone Pilato. Kwa kuwa Pilato hakujali maswali ya kidini, basi sasa Wayahudi kwa ujanja wao wanabadilisha shtaka lao kuwa la kisiasa kwamba Yesu amedai ufalme (m.2, Pilato akamwuliza, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi? Yesu akajibu, akamwambia, Wewe wasema). Maana yake anataka kuwapindua Warumi. Pilato mwenyewe hakuona kosa ila kwa kutokuwa na msimamo alikubali kumhukumu Yesu. Pilato akitaka kuwafurahisha watu tu, anashindwa kutoa uamuzi wa haki. Yesu anakubali mateso kuwa sehemu ya utumishi kwa Mungu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz