Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021Mfano
Mtume Paulo hajawahi kutembelea usharika wa Kolosai (2:1, Nataka ninyi mjue jinsi ilivyo kuu juhudi yangu niliyo nayo kwa ajili yenu, na kwa ajili ya wale wa Laodikia, na wale wasioniona uso wangu katika mwili). Kwa maelezo ya Epafra (m.7-8, Kama mlivyofundishwa na Epafra, mjoli wetu mpenzi, aliye mhudumu mwaminifu wa Kristo kwa ajili yenu; naye alitueleza upendo wenu katika Roho) amepata kufahamu kwamba Wakristo wamekua katika imani, lakini pia amesikia kwamba kuna hatari fulani. Kwa hiyo ameamua kuwaandikia barua hii ili awasaidie. Anaanza na salamu na kujitambulisha mbele yao kwamba yeye ni mtume wa Yesu. Baada ya hapo anafundisha kwamba kuna uhusiano mkubwa kati ya imani, upendo na tumaini (m.3-5a, Twamshukuru Mungu, Baba yake Bwana wetu Yesu Kristo, siku zote tukiwaombea; tangu tuliposikia habari za imani yenu katika Kristo Yesu, na upendo mlio nao kwa watakatifu wote; kwa sababu ya tumaini mlilowekewa akiba mbinguni). Kumbuka kwamba kumshukuru Mungu huimarisha imani yako. Basi tufuate mfano wa Paulo: Twamshukuru Mungu, Baba yake Bwana wetu Yesu Kristo, siku zote tukiwaombea (m.3).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz