Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021

SIKU 30 YA 31

Injili ni siri, yaani, haijitokezi moyoni mwa mtu bali inafunuliwa na Roho Mtakatifu. Ndivyo ilivyo hadi leo. Kwa hiyo ni kazi ya Wakristo kumtangaza Yesu Kristo ili isiwe siri, bali iwe habari njema kwa kila mtu. Mungu kwanza alimtumia Paulo, na kwa njia hii hata sisi tumepata kuisikia habari ya neema. Sasa Mungu anataka atutumie sisi tuliopo duniani kwa ajili ya kueneza Injili kwa watu wote, wala si kwa kabila letu tu. Na katika hili, vipawa vyetu ni tofauti. Zingatia maelezo katika 1 Kor 12:1-4, Ndugu zangu, kwa habari ya karama za roho, sitaki mkose kufahamu. Mwajua ya kuwa mlipokuwa watu wa Mataifa, mlichukuliwa kufuata sanamu zisizonena, kama mlivyoongozwa. Kwa hiyo nawaarifu, ya kwamba hakuna mtu anenaye katika Roho wa Mungu, kusema, Yesu amelaaniwa; wala hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu. Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule.

siku 29siku 31

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz