Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021Mfano
Mwili bila kichwa hauna uhai. Mwili ni mfano wa kanisa, na Yesu Kristo ni kichwa cha mwili huu (m.18, Ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha Kanisa). Kwa hiyo kanisa si sawa na askofu, mchungaji au jengo fulani. Kanisa lipo pale ambapo watu wamepata kuungana na Yesu Kristo kwa njia ya imani yao. Kumbuka Yesu anavyosema katika Yn 15:4-5, Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote. Hapo ndipo kuna uhai, na kwa sababu ya uhai huo Wakristo wanapenda wakusanyike, kusikia Neno la Mungu na kumsifu Yesu Kristo. Maelezo zaidi kuhusu Yesu Kristo kama kichwa chetu yanafuata katika m.19-20: Katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae; na kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi, au vilivyo mbinguni.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz