Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021

SIKU 29 YA 31

Mpango wa Mungu kuhusu wokovu umekamilika. Kwa njia ya Yesu Kristo upatanisho kati ya Mungu na sisi umefanyika. Lakini tuko wapi? Jipime kwa kusoma m.23a: Mkidumu tu katika ile imani, hali mmewekwa juu ya msingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia habari zake. Jambo lililo muhimu kwetu linapaswa kuwa sawa sawa na jambo lililo muhimu kwa Mungu (kama Paulo anavyoshuhudia katika m.25, Nimefanywa mhudumu wake, sawasawa na uwakili wa Mungu, niliopewa kwa faida yenu, nilitimize neno la Mungu), maana hatujafika mbinguni bado. Majaribu ni mengi, lakini tusikate tamaa, bali tusimame imara katika Yesu. Mkristo anashinda dhambi zake kwa njia ya Yesu, maana Yesu ameshinda tayari kwa ajili yetu. Yeye ni mpatanishi wetu. 

siku 28siku 30

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz