Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021

SIKU 27 YA 31

Palikuwepo walimu wa uongo katika usharika wa Kolosai, na waliingiza mafundisho maharibifu. Walimtangaza Yesu Kristo kuwa malaika, na kwa njia hii walimkana kuwa siye Mungu. Kwa hiyo Paulo anakaza kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu na aliyetuokoa. Je, umekubali kuondolewa na Yesu Kristo kutoka katika nguvu za giza? Ameshatuokoa - je, umeupokea wokovu wake? Yesu Kristo anatosha. Katika ufalme wa Mungu tu kuna usalama. Yesu Kristo ni Mungu kweli. Angalia kwa makini sifa zake katika m.15-16: Ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote. Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake.

siku 26siku 28

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz