Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021Mfano
Kuna watu wanaoonyesha mateso ya Yesu kwa hatua tisa: Kuhuzunika, kupigwa makofi, kupelekwa kwa Pilato, kupigwa mijeledi, kutiwa taji la miiba, kusulubishwa, kupigiliwa misumari, kupaza sauti kwa Mungu: "Mbona umeniacha?" na "Imekwisha". Lengo la kifo chake ni kuukomboa ulimwengu. Wahalifu wawili wanasulubiwa pamoja naye. Zingatia Lk 23:39-40, jinsi kila mmoja anavyotoa maneno au anavyotumia dakika zake za mwisho: Mmoja wa wale wahalifu waliotungikwa alimtukana, akisema, Je! Wewe si Kristo? Jiokoe nafsi yako na sisi. Lakini yule wa pili akamjibu akamkemea, akisema, Wewe humwogopi hata Mungu, nawe u katika hukumu iyo hiyo? Je, wewe unatoa maneno gani kwa kifo cha Yesu. Unalingana na mhalifu yupi?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz