Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021

SIKU 22 YA 31

Saa tisa Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Maana yake, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha? Mlio huu katika m.34 unaonyesha ukali wa mateso ya Yesu. Baada ya kufa kwake, mambo mawili yalitokea: 1. Nchi ilikuwa na giza kwa masaa matatu ya mchana. 2. Pazia la hekalu lilipasuka. Hili laonyesha kwamba nafasi ya kuingia patakatifu pa Mungu sasa ipo wazi. Kristo ametutengenezea njia. Hakuna pazia linalotuzuia. Kwa maana kwa yeye sisi sote tumepata njia ya kumkaribia Baba katika Roho mmoja (Efe 2:18). Sasa tunaweza kumkaribia Mungu katika maombi, na baada ya maisha ya hapa duniani tunakaribishwa kwake. Yesu amepata mateso haya ili atukomboe kwenye hatari ya kifo cha milele.

siku 21siku 23

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz