Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021

SIKU 5 YA 31

Somo hili linataka kutufundisha jambo la utakatifu. Ezekieli anaona vitu vitakatifu mbalimbali (m.13-14, Vyumba vya upande wa kaskazini, na vyumba vya upande wa kusini, ambavyo vyaelekea mahali palipotengeka, ni vyumba vitakatifu; humo makuhani, wamkaribiao Bwana, watakula vitu vilivyo vitakatifu sana; humo wataviweka vitu vilivyo vitakatifu sana …) na ukuta wa kutenganisha eneo takatifu na lile la kawaida (m.20, lilikuwa na ukuta pande zote, urefu wake mianzi mia tano, na upana wake mianzi mia tano, ili kupatenga mahali palipo patakatifu, na mahali palipo pa watu wote). Sisi tuko upande gani wa ukuta huo? Tunapomwamini Yesu na kubatizwa, Roho Mtakatifu anaingia na kukaa kwetu, naye anaendelea kututakasa. Hivyo tunawezeshwa kuishi maisha matakatifu. Lakini afichaye dhambi zake, anamhuzunisha Roho na hatimaye anamfukuza. Tunaoneshwa hekalu jipya ili tuyatahayarikie maovu yetu (43:10).

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz