Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021

SIKU 9 YA 31

Masharti yote yalenga kufundisha utakatifu. Zingatia Mungu anavyosema juu ya watumishi wa hekalu katika m.23: Watawafundisha watu wangu tofauti iliyopo kati ya vitu vitakatifu na vitu vya sikuzote, na kuwafundisha kupambanua kati ya yaliyo machafu na yaliyo safi. Kila ahudumuye nyumbani kwa Bwana ajue kuwa anahudumia mahali patakatifu. Huduma yake isichanganywe na uovu wowote. Mhudumu yeyote aliyeanguka katika dhambi, kama ataendelea kuhudumu bila kujitakasa kwanza, basi atakuwa anaitafuta ghadhabu ya Mungu (m.10, Walawi waliofarakana nami, hapo Waisraeli walipopotea, waliopotea na kuvifuata vinyago vyao, watachukua uovu wao wenyewe). Ni lazima atakaswe; na hata hivyo inawezekana hataweza kurudi tena katika huduma hiyohiyo (m.13, Wala hawatanikaribia, kunihudumia katika kazi ya ukuhani, wala hawatakaribia vitu vyangu vitakatifu kimojawapo, vitu vilivyo vitakatifu sana; bali watachukua aibu yao, na machukizo yao yote waliyoyatenda). Zingatia neno la Mungu kwa wahudumu wake: Mimi ni urithi wao na milki yao (m.28).

siku 8siku 10

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz