Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021

SIKU 13 YA 31

Mungu anatimiza ahadi ya kuwapa Israeli nchi ya ahadi kuimiliki. Kwanza anaonesha mipaka ya nchi iliyokombolewa (47:13-23), kisha mgawanyo wa koo ndani ya nchi husika (48:1-29). Mipaka hulingana na nchi ya Kanaani kama mipaka yake ilivyo (ukipenda unaweza kulinganisha na Hes 34:1-12). Kati ya majina mengi ya mahali na ya watu, tukumbuke habari mbili: 1) Nchi itagawanywa sawa kati ya watu: Mtaimiliki, mtu huyu sawasawa na huyu (m.14). 2) Kutakuwa na nafasi kwa wageni: Itakuwa, mgeni akaaye katika kabila iwayo yote, atapewa urithi katika kabila asema Bwana MUNGU (m.23) – kama sisi ambao sio Waisraeli kwa kuzaliwa. Bwana asifiwe kwa huruma yake.

siku 12siku 14

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz