Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021Mfano
Somo lote linaonyesha mabadiliko mema yanayotokana na utukufu wa Bwana kulijaza hekalu, yaani nyumba yake Mungu. Hakuna atakayenyang’anywa nafasi yake mahali hapo. Mfalme hatawaondolea watu urithi wao kama ilivyotokea zamani (m.18, Mkuu hatawaondolea watu urithi wao, hata kuwatoa kwa nguvu katika milki yao; atawapa wanawe urithi katika mali yake mwenyewe, watu wangu wasije wakatawanyika, kila mtu mbali na milki yake). Sadaka zitachemshwa mahali pake. Na mwisho kuna habari njema ya mto ya hekalu. Kila kitu kitaishi po pote utakapofikilia mto huo (m.9). Maji yake yataleta ustawi mzuri na uponyaji (m.12, Utamea kila mti wa chakula, ambao majani yake hayatanyauka, wala matunda yake hayatatindika kamwe; utatoa matunda mapya kila mwezi, kwa sababu maji yake yanatoka mahali patakatifu; na matunda yake yatakuwa ni chakula; na majani yake yatakuwa ni dawa). Ndivyo itakavyokuwa kwa sababu Bwana yupo hapa (48:35).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz