Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021Mfano
Kama ilivyo katika 45:1-8 Mungu anakumbusha tena katika 48:8-14 kutenga eneo kwa ajili ya Bwana. Hapo ni mahali pa kujenga hekalu na maeneo kwa makuhani, Walawi na mfalme. Kuna neno linalokazwa mara nne (m.8, 10, 15 na 21): Mahali patakatifu pa Bwana patakuwa katikati yake. Ujumbe ni wazi, tena mwema sana. Tunapewa picha ya Yerusalemu mpya baada ya Mungu kumaliza kazi yake ya ukombozi: Jina la mji huo tangu siku hiyo litakuwa hili, BWANA yupo hapa. Je, wewe pia utakuwepo hapo?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz