Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021Mfano
Ilipofikia saa ya kukamatwa kwa Yesu, wanafunzi walikimbia. Yuda akamsaliti Yesu kwa kumbusu. Kumbuka maneno ya Yesu juu ya mtu atakayemsaliti katika Mk 14:21, Mwana wa Adamu aenda zake kama alivyoandikiwa; lakini ole wake mtu yule ambaye amsaliti Mwana wa Adamu; ingekuwa heri kwake mtu yule kama asingalizaliwa. Yesu anawashangaa wanapomjia na silaha kama kumkamata mtu mnyang’anyi. Maana silaha zao hazina uwezo wowote juu yake. Ila upendo wake kwa wanadamu ndio unaomfanya awe mpole ili andiko litimie, kama ilivyoandikwa katika Isa 53:12, Alimwaga nafsi yake hata kufa, akahesabiwa pamoja na hao wakosao. walakini alichukua dhambi za watu wengi, na kuwaombea wakosaji. Mara nyingi sisi wanadamu wakati wa mateso ni waoga na tunakata tamaa ya kuendelea mbele, lakini Yesu anao ujasiri wa kusonga mbele.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz