Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021

SIKU 16 YA 31

Pasaka ilitanguliwa na mlo wa jioni. Hapo Yesu alieleza hasara ya mtu atakayemsaliti. Yuda anasikia maneno haya bila kushtuka na kuomba msaada kwa Yesu. Moyo wake umekuwa mgumu sana. Wewe je, Yesu anapokuonya juu ya dhambi, nawe unapuuzia? Upuuzi huu utakupeleka Jehanamu, na ni heri usingalizaliwa kuliko hayo mateso. Mwili na damu ya Yesu ni mwanzo wa agano jipya kati ya Mungu na mwanadamu. Je, kuna kitu kinachokutenga kuwa mshiriki wa mwili na damu ya Yesu Kristo, aliyejitoa kwa ajili yako?

siku 15siku 17

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz