Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021Mfano
Utukufu wa Mungu ulijaza hekalu. Ni ishara ya utakatifu wa Mungu na mahali akaapo panavyotakiwa kuheshimiwa na kutunzwa kwa ibada. Hii yatufundisha Wakristo mambo kadhaa: 1) Ni kuishi maisha matakatifu ikiwa tunaheshimu kuwa sisi ni wateule wa Mungu na Roho wa Mungu anakaa ndani yetu. 2) Ni kuchagua vema watu wa kutumika kanisani bila kujali kama ni wainjilisti, wachungaji, wafanya usafi au waimbaji. Tuzingatie kuwa hao wote wanakwenda mbele za Bwana, hivyo wawe Wakristo wa moyo (m.9, Bwana MUNGU asema hivi, Hapana mgeni, ambaye moyo wake haukutahiriwa, wala mwili wake haukutahiriwa, atakayeingia patakatifu pangu, miongoni mwa wageni walio kati ya wana wa Israeli).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz