Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021Mfano
Ukamilifu wa hekalu takatifu la Mungu ni pamoja na uwepo wa madhabahu. Mungu ana neno maalumu kuhusu mahali hapo: Kwa muda wa siku saba wataifanyia madhabahu upatanisho, na kuitakasa; ndivyo watakavyoiweka wakfu (m.26). Kwa sababu ya dhambi za Waisraeli, ilibidi madhabahu itakaswe kamili kabla ya kutumika kwa sadaka zao. Ndivyo sheria za agano la kale zilivyodai. Kwa mtazamo wa agano jipya la Kristo, maana yake ni hii: Kwa toleo moja Yesu ametukamilisha hata milele sisi tunaotakaswa (Ebr 10:14, Maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa). Kwenye msingi huu, tunaweza kumtolea miili yetu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu (Rum 12:1). Basi, tumwabudu!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz