Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021

SIKU 6 YA 31

Mungu alijiondoa kwa taifa la Israeli lilipomwasi. Angalia mfululizi wa matukio katika mistari ifuatayo: Utukufu wa Bwana ukapaa kutoka kwa kerubi yule, ukasimama juu ya kizingiti cha nyumba (10:4). Kisha huo utukufu wa Bwana ukatoka pale juu ya kizingiti cha nyumba, ukasimama juu ya makerubi. Nao makerubi wakainua mabawa yao, wakapaa juu kutoka katika dunia machoni pangu, hapo walipotoka nje, nayo magurudumu yakawa kando yao; wakasimama mahali pa kuingilia pa mlango wa upande wa mashariki wa nyumba ya Bwana; na utukufu wa Mungu wa Israeli ulikuwa juu yao (10:18-19). Utukufu wa Bwana ukapaa juu toka katikati ya mji, ukasimama juu ya mlima wa upande wa mashariki wa mji (11:23). Sasa Ezekieli anashuhudia jinsi Mungu anavyolirudia hekalu lake, Mungu akisema, Nitakapokaa kati ya wana wa Israeli milele (m.7). Inawezekanaje? Je, Waisraeli wamejitengeneza? Mungu anatoa jibu la msingi katika 39:25, Sasa nitawarejeza. Zingatia mstari wote: Bwana MUNGU asema hivi, Sasa nitawarejeza watu wa Yakobo waliohamishwa, nitawahurumia nyumba yote ya Israeli; nami nitalionea wivu jina langu takatifu. Lakini pia Waisraeli hutakiwa kufanya kitu: Basi sasa wayaondoe mambo yao ya kikahaba, na mizoga ya wafalme wao, yawe mbali nami, nami nitakaa kati yao milele (m.9). Kufunuliwa hekalu jipya hutusaidia kuyatahayarikia maovu yetu, yanayowekwa wazi tukikutana na utakatifu wa Mungu. Ndivyo Mungu anavyomwambia Ezekieli katika m.10: Wewe, mwanadamu, waonyeshe wana wa Israeli nyumba hii, ili wayatahayarikie maovu yao; na waipime hesabu yake.

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz