Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022

SIKU 12 YA 31

Katika kukamilisha ujenzi wa majengo yake ya fahari, Sulemani aliazima dhahabu kiasi cha kilo kama elfu mbili hivi kutoka kwa Hiramu. Ili kulipa madeni hayo Sulemani alimpa Hiramu miji ishirini kaskazini mwa Israeli. Bahati mbaya Hiramu hakuridhika na miji hiyo, akairudisha. Ndipo ikamlazimu Sulemani kutafuta njia nyingine kumlipa. Desturi ya kuazimana vitu au fedha ilikuwepo tangu zamani. Hata leo Wakristo tunaazima fedha. Tukumbuke tu twapaswa kuwa na mipango mizuri ya kufanya marejesho.

siku 11siku 13

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Agosti pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Zakaria. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/