Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022

SIKU 13 YA 31

Sulemani aliweza kufanya biashara. Ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa akaunda merikebu. Na kwa kuwa Waisraeli hawakuwa mafundi sana kwa habari ya kazi za ubaharia, Sulemani akaendeleza urafiki wake na Hiramu kwa kukodi mabaharia kutoka Tiro ili wawafundishe ubaharia Waisraeli. Kwa njia ya kutumia merikebu hii kwa ushirikiano, Sulemani na Hiramu wakafaulu kupata faida ya pamoja. Hili litufundishe kuwa, Mungu alituumba na karama tofautitofauti ili tushirikiane. Tushirikiane ili kufaidiana.

siku 12siku 14

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Agosti pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Zakaria. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/