Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022

SIKU 14 YA 31

Hekima ya Mungu ndani ya Sulemani ilienea hadi nchi za mbali. Wengi wakatamani kuja kwa Sulemani kujifunza na kuthibitisha hayo waliyoyasikia, Malkia wa Sheba akiwa mmoja wao. Hapa tujifunze kwamba ukimruhusu Mungu aongoze hekima, karama na vipawa vyako, watu watakutafuta kwa gharama yoyote ili uwasaidie. Tambua kuwa kama Mungu ameweka jambo zuri ndani yako, ni kwa ajili ya Yeye Mungu kujitukuza kwa wengine. Kwa hiyo kila tufanyalo, kwa neno au kwa tendo, tuhakikishe Mungu anatukuzwa.

siku 13siku 15

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Agosti pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Zakaria. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/