Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022

SIKU 15 YA 31

Mafanikio na fahari ya Sulemani inatufundisha kuwa Mungu anatutakia mema. Nchi na vyote viijazavyo ni mali yake. Kama sisi ni watoto wake, basi tu warithi wa fahari hizo. Tukumbuke tu kupokea wema wake kwa unyenyekevu, tukimtegemea Yeye kwenye mipango na utendaji wetu wote. Ukimtumikia Mungu kwa kumtanguliza, unampa nafasi ya kukufanikisha katika shughuli zako na mipango yako mbalimbali. Hata hivyo tusiishi kwa kutegemea miujiza wala utajiri, bali tufanye kazi kwa bidii pamoja na Mungu.

siku 14siku 16

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Agosti pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Zakaria. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/