Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022Mfano
Behewa kubwa pande zote ilikuwa na safu tatu za mawe ya kuchongwa, na safu moja ya mihimili ya mierezi; mfano wa behewa ya ndani ya nyumba ya Bwana, na ukumbi wa nyumba. Mfalme Sulemani akatuma watu kumleta Huramu kutoka Tiro (m.12-13). Tukianzia hapo, tunaona kuwa fundi aliyeletwa kutoka Tiro ndiye anayeendeleza kazi nzuri ya kulipamba hekalu kwa kujenga nguzo ndefu za mapambo na kuweka mifano ya nyuzi, mataji, nyavu na makomamanga 200. Hata leo tunapotaka kujenga kanisa, tutafute mafundi stadi, hata kama watapatikana mbali kwa gharama. Kazi ya ujenzi wa kanisa au jengo la watumishi wa kanisa iwe na ubora na mvuto hata kuzidi nyumba zetu. Maana kwa kufanya hivyo tunamfanya Mungu kuwa namba moja na wa thamani kuliko mambo yetu yote.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Agosti pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Zakaria. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/