Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022

SIKU 5 YA 31

Kama ilivyoandikwa katika 8:65, watu wengi walifika kutoka sehemu mbalimbali ili kulizindua hekalu: Wakati ule Sulemani akafanya sikukuu, na Israeli wote pamoja naye, kusanyiko kubwa sana, kutoka maingilio ya Hamathi mpaka kijito cha Misri, mbele za Bwana, Mungu wetu, siku saba na siku saba, yaani siku kumi na nne. Walawi tu ndio waliotumika kuhamisha sanduku la agano na vyombo vitakatifu viingie hekaluni, maana hao ndio walioteuliwa na Mungu kutumika hekaluni. Taratibu zote zilifuatwa ili kuliweka wakfu hekalu. Wingu lile liliposhuka, ni ishara ya Mungu kukubali kukaa katikati ya watu wake (m.10-11,Ikawa, makuhani walipotoka katika patakatifu, nyumba ya Bwana ikajaa wingu; hata makuhani hawakuweza kusimama ili kufanya huduma yao, kwa sababu ya wingu lile; kwa kuwa nyumba ya Bwana ilikuwa imejaa utukufu wa Bwana). Kanisani pia kuna taratibu. Tusimkosee Mungu kwa kuzikiuka na kusababisha kwamba hataweza kukaa kwetu. Mungu ni Mungu wa amani.

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Agosti pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Zakaria. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/