Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022

SIKU 4 YA 31

Vyombo vyote vya shaba vilivyowekwa hekaluni, Sulemani hakutaka hata ijulikane thamani yake, maana ilikuwa kubwa sana (7:47, Sulemani akaviacha vyombo vyote visipimwe kwa kuwa vilikuwa vingi mno; wala uzito wa shaba haukujulikana). Hapa anatufundisha kuwa kama tumeamua kufanya kazi kwa ajili ya Mungu, tuifanye kwa ubora na thamani kubwa, maana nchi na vyote viijazavyo ni mali yake, hivyo hatuna sababu ya kumwekea mipaka ya ubora Mungu wetu. Hata tukiamua kutoa sadaka, tutoe yenye ubora na thamani kubwa, hata kama itazidi fungu la kumi. Cha msingi ni kutoa kwa moyo wa kumpenda na kumshukuru Mungu.

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Agosti pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Zakaria. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/