Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022

SIKU 9 YA 31

Hekalu ni nyumba ya misheni. Sulemani anatukumbusha kuwa na ushuhuda mzuri kwa watu wote ikiwa ni pamoja na kwa wageni, ili kupitia kwetu wamfahamu Mungu na wokovu wake. Maana yake, neema ya Mungu imefunuliwa kwa watu wote. Sisi tulio Wakristo tusiiwekee mipaka kana kwamba neema hiyo ni ya Wakristo tu. M.44-45 inatuambia kwamba zinatokea vita za kupambana na nguvu za uovu: Ikiwa watu wako watoka kwenda kupigana na adui zao, kwa njia yo yote utakayowapeleka, wakikuomba, Bwana, kuuelekea mji huu uliouchagua, na nyumba hii niliyoijenga kwa jina lako; basi, uyasikie huko mbinguni maombi yao na dua yao, ukaitetee haki yao. Hata hapo tusitegemee nguvu yetu, bali tuombe Mungu wa kweli atutetee. Kwa ujumla Sulemani anaomba Mungu awapokee hekaluni watu wote na kuwajibu.

siku 8siku 10

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Agosti pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Zakaria. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/