Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022

SIKU 8 YA 31

Kama kanisani, hekalu lilikuwa mahali pa maombi. Hivyo Sulemani aliomba Mungu apokee sala za watakaokuja kuabudu kwenye madhabahu, mahali pa upatanisho na msamaha. Hii itufundishe kuzipeleka dhambi zetu na changamoto za maisha yetu kwa Mungu tukitegemea upatanisho aliotufanyia Yesu. Hapo ndipo penye majibu. Sulemani anataja waliokosana, waliotenda dhambi, taifa kupigwa na adui, kukosekana kwa mvua, baa la njaa, magonjwa, nzige n.k. Tulete yote kwa Mungu tukikumbuka anaijua mioyo yetu, kama Sulemani anavyomwambia Mungu katika m.39: Usikie huko mbinguni, makao yako, ukasamehe, ukatende, ukampe kila mtu kwa kadiri ya njia zake; wewe ujuaye moyo wake; (maana wewe peke yako ndiwe uijuaye mioyo ya wanadamu wote).

siku 7siku 9

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Agosti pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Zakaria. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/