Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022

SIKU 7 YA 31

Mfalme Sulemani akapiga magoti ili kumwabudu Mungu kwa unyenyekevu na kuomba mbele za watu wote (2 Nya 6:13b, akapiga magoti mbele ya mkutano wote wa Israeli, akaikunjua mikono yake kuelekea mbinguni). Kwa unyenyekevu anaonesha kuwa yeye na Daudi, baba yake, walipewa neema ya kumjengea Mungu hekalu. Ndipo anaomba neema hiyo iendelee kutenda kazi hapo katika hekalu, ikawaguse watakaolitumia. Hapa tunauona unyenyekevu wa Sulemani. Pamoja na kufanya jambo hilo kubwa, bado anaona ni kwa neema tu amewezeshwa. Tujifunze kuwa wanyenyekevu kwa Mungu, hata kama tumefanikiwa sana maishani.

siku 6siku 8

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Agosti pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Zakaria. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/