Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022

SIKU 6 YA 31

Utukufu wa Bwana hukaa mahali anapopewa heshima na utukufu na Neno lake linapopokelewa kwa utiifu wa imani. Baada ya kukamilisha ujenzi na Mungu kujidhihirisha kwao, Mfalme Sulemani akawashukuru makutano wote, akawabariki mkutano wote wa Israeli (m.14), kisha akamshukuru na kumtukuza Mungu. Hili litufundishe kwamba Mungu akijidhihirisha kwenye kazi au maishani mwetu, tusijitwalie utukufu bali tumrudishie sifa na utukufu wote. Aidha kama viongozi tunapofanikisha kazi fulani, tukumbuke kuwashukuru wote waliohusika kuifanikisha.

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Agosti pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Zakaria. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/