Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kusaka UkuuMfano

Kusaka Ukuu

SIKU 1 YA 7

Mwanamume wa Kifalme

Kama mwanamume, wewe ndiye kiongozi. Iwe wataka au hutaki. Ikiwa u mwanamume, upende usipende, wewe ni kiongozi kwa wadhifa. Inawezekana utekelezi wako sio mzuri hata kidogo, ila umeitwa katika wadhifa huo uongoze. Hiyo ndio inajumuisha mwito wa kiadamu. Mungu alimuumba Adamu mbele ya Hawa kwa sababu wajibu wake ulikuwa uwe wa utawala nakuongoza. Adamu alipewa mwito wake wa kutunza na kuiangalia bustani hata kabla ya Hawa kuumbwa. Kwa msingi huo, ilikuwa ni Adamu ndiye Mungu alimtafuta wakati ambapo wote wawili, Adamu na Hawa walikosa kumtii.

Hii ni kwa kuwa Adamu aliwajibika kikamilifu. Kama mwanamume, unawajibika kikamilifu kwa wale walio katika milki yako. Jinsi unavyoongoza itachangia pakubwa iwapo itakuwa ni baraka au mauti kwa wale walioko katika eneo unalo ongoza. Waweza kuwaongoza walioko chini ya uangalizi wako kufikia mahali penye ufanishi, au waweza kuwaelekeza walioko chini ya angalizi wako penye fujo. Ni wajibu wako jinsi utakavyo eneo lako liwe.

Ila kuongoza vyema si jambo ufanyalo kwa siku moja kisha ukasahau yote kuihusu. Kutawala vyema ni ujuzi wa maisha ulioandaliwa katika mioto ya uaminifu na kujitolea. Huongozi vyema kwa kudhani kuwa ni jambo la heshima sana kufanya. Ili uwe mwanamume wa kifalme kama ulivyoumbwa, ni lazima uwajibike siku baada ya nyingine – mwaka baada ya mwingine – muongo baada ya mwingine, kwa kukusudia na daima ukijitolea kuongoza milki yako vyema.

Kujitolea kwako kukidhi matarajio ya wale unaowaongoza kunapaswa kuwatia moyo wale waliokabidhiwa kwa uangalizi wako kuishi katika kiwango kikubwa zaidi cha kujitolea katika kutimiza kile ambacho Mfalme wa Ulimwengu amewaitia kufanya. Siku zote kumbuka kuwa siku nyingi za baadaye zitaamuliwa na jinsi unavyoongoza vyema leo.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Kusaka Ukuu

Wanaume hutamani kuwa wakuu. Sio tu kwamba tunatamani kuwa wakuu, bali pia tunatamani kutambuliwa kuwa wakuu. Lakini wanaume wengi hutatatizika wanapotaka kunufaika na uwezo wao wa kweli nao huishia kukimbizana na mambo yanayowapeleka mbali zaidi na pale wanapotaka kuwa. Gundua uanaume halisi na Tony Evans.

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/