Kusaka UkuuMfano
Mwanamume wa Kifalme
Wanaume hutamani kuwa wakuu.
Sio tu kwamba tunahamu ya kuwa wakuu, lakini tunahamu ya kutambuliwa kuwa wakuu. Hakuna mchezaji aliye kwenye timu iliyoshinda katika ubingwa wa michezo wa vikapu ya NBA ambaye hukataa kupokea pete au medali yake. Huidai na kuivaa ili kila mmoja ajue alichotenda. Kwa kweli, kuna wanaume walioshinda ubingwa huo miaka ishirini iliyopita ambao hadi sasa huvaa pete zao. Japo muda mwingi umepita, wao huvaa kwa sababu wanataka wengine wajue kwamba wao ni wakuu.
Kwa kweli, ni kuu sana shauku ya mwanamume ya kuwa mkuu kiasi kwamba mara kwa mara atajaribu kupata kwa uzoefu wa mtu mwingine. Njia ya kawaida kuona hili, ni hapo mwanamume anapovalia jezi lenye jina la mwanamume mwingine. Iwapo tutajisikia kufarijika vya kutosha kwa kiwango cha kukubali hili katika nyanja za kiroho au la, wanaume wanataka kuwa wakuu.
Mimi nitakubali, sijali – Nataka kuwa mkuu.
Na ikiwa utakuwa wazi kabisa na mkweli, ningeweka dau kuwa unataka kuwa mkuu pia.
Lakini kile ambacho chaweza kukushangaza, na ninachotaka nipendekeze ni kwamba, mbali na kile tunachosikia kila mara kuhusu mafundisho ya Biblia ya utumishi na unyenyekevu, Mungu ataka uwe mkuu pia.
Sio tu kwamba Mungu anataka uwe mkuu katika ufalme wake, ameiweka kuwa ni hatima yako.
Ukuu ni kutumia uwezo wako kikamilifu kwa utukufu wa Mungu na kwa ajili ya wema wa wengine. Paulo anahimiza waumini wenzake “wazidi kuwa bora zaidi” kwa jinsi wanavyotii amri zake Mungu katika maisha yao. Kwa Wakorintho, aliwasihi “wazidi sana kutenda kazi ya Bwana siku zote.”Aliwahimiza kutafuta kuwa wakuu katika yote waliyotenda, kulingana na 1 Wakorintho 10:31, na wafanye yote kwa utukufu wa Mungu na kulifanya jina lake kuwa kuu.
Wanaume, nawataka muwe na uzoefu wa kweli hii kabisa.
Nisikie ninapo sema hivi – ni sawa kutaka ukuu. Hilo si jambo unalohitaji kununguna wakati ambapo hakuna mmoja anyesikia, au kuchungulia kwenye mlango wa nyumba ya kanisa. Yaweza isikubaliane na kile umesikia kuwa kama mwito wa kuwa mpole, mnyenyekevu na kuwa mtumishi kwa wote, ila katika uhalisia wote, ukuu haubatili yoyote katika hayo. Kwa kweli, ukuu halisia yajumuisha ufafanuzi wa kweli kuhusu hayo yote.
Kuhusu Mpango huu
Wanaume hutamani kuwa wakuu. Sio tu kwamba tunatamani kuwa wakuu, bali pia tunatamani kutambuliwa kuwa wakuu. Lakini wanaume wengi hutatatizika wanapotaka kunufaika na uwezo wao wa kweli nao huishia kukimbizana na mambo yanayowapeleka mbali zaidi na pale wanapotaka kuwa. Gundua uanaume halisi na Tony Evans.
More
Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/