Kusaka UkuuMfano
Mwanamume wa Kifalme.
Mojawapo ya vipengele vyenye umuhimu katika kuendeleza ufalme wa Mungu ni katika ufahamu kwamba wewe kama mwanamume, wawajibika kwa yote yakuangukiayo kwenye eneo lako la ushawishi ambalo Mungu amekupa. Mwanamume anayeachilia wajibu wake katika fujo au mtafaruku ulioko katika eneo lake, iwe yatokana moja kwa moja na matendo yake au la, huwa amejizuia mwenyewe kuokoa hali hiyo. Sio tu kwamba anakosa nguvu za Mungu za kusonga mbele, bali amejiondoa mwenyewe hata kurekebisha kile kilichovunjika.
Mimi ni mchungaji wa kanisa lililoimarika lenye wafanya kazi zaidi ya 200. Mara nyingi shughuli za kanisa huendelea kwa njia nyororo. Lakini mara nyingine naweza kupokea simu kutoka kwa mtu ambaye anasikika amekasirishwa, akiniambia kuhusu jambo ambalo hakulipenda
Sitasahau wakati ambapo mwanamke mmoja alipiga simu aniambie kwamba alikuwa amepiga simu ya kanisa mara tano siku iliyopita na hakuweza kumpata mpokeaji simu wakati wowote ule. Kila mara mwanamke huyo alipiga simu kanisani, mpokeaji hakuwepo ili kujibu, kwa hivyo simu yake iliingia kwenye ujumbe wa sauti.
Mitikio wangu wakawaida ungekua kumuuliza kwa nini asimpelekee mpokeaji simu malalamiko yake, na kwa nini ananiletea mimi? Mimi ndiye mchuangaji mkuu, hata hivyo, kuna wafanya kazi mia kadhaa wanaoendesha shughuli za kanisa, shule ya Kikristo na kituo cha uhamasishaji. Je! Ninapaswa kujua kwa nini mpokeaji simu hakuwepo wakati huo Huenda alikuwa kwenye simu nyingine. Bila kukukasirisha, tafadhali muulize.
Ijapokuwa ndivyo nilijihisi kusema, kwa hakika hilo si ndilo nalisema. Kwa sababu, katika kweli yote, mpiga simu yu sahihi. Amefuatilia na kumpata huyo atakayeshughulikia malalamiko yake.
Kama mchungaji mkuu, huenda siwezi kulaumiwa moja kwa moja kuhusu kutokuwepo kwa anayepokea simu, lakini wadhifa wangu waniwajibisha kikamilifu. Hivyo basi, nilipopokea simu ile, niliishughulikia mara moja. Kwa nini? Kwa sababu mimi ndiye niwajibika kikamilifu kuhakikisha kwamba jambo hilo halitatokea tena.
Malalamiko yafananayo na haya ndiyo yaliletwa kwa Adamu. Si kuhusu simu iliyopigwa, bali kuhusu kipande cha tunda. Swali lilielekezwa kwa Adamu pasipo kuangalia ni nani aliyetenda nini wa kwanza, yeye ndiye alikuwa na wajibu timilifu. Hii ni kwa kuwa, Adamu aliwajibika chini ya Mungu kama mwakilishi kutenda na kuhakikisha kwamba ajenda yake Mungu imetekelezwa.
Kuhusu Mpango huu
Wanaume hutamani kuwa wakuu. Sio tu kwamba tunatamani kuwa wakuu, bali pia tunatamani kutambuliwa kuwa wakuu. Lakini wanaume wengi hutatatizika wanapotaka kunufaika na uwezo wao wa kweli nao huishia kukimbizana na mambo yanayowapeleka mbali zaidi na pale wanapotaka kuwa. Gundua uanaume halisi na Tony Evans.
More
Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/