Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kusaka UkuuMfano

Kusaka Ukuu

SIKU 4 YA 7

Mwanamume wa Kifalme

Hakuna nipendacho sana katika maisha kuliko kuwa mwanamume. Nampenda mke wangu, familia yangu na mwito wangu – lakini yote haya yanautimilifu wake katika uhalisia mkuu – wa kuwa mwanamume. Wakati mwingine niamkapo asubuhi kabla kuiweka miguu yangu kwenye sakafu, hujiambia, “Evans, ni jambo kuu kuwa mwanamume.” Siku nzima yasonga mbele ikisubiri niigundue, niwe na uzoefu wayo, na kuishinda.

Kuna kitu cha asili katika kinasaba cha uanaume kinachowahimiza kujitokeza kutatua maswala tata, kulinda, kutetea, kushinda na kurejesha. Changamoto za maisha hutuchokoza ili tuzipinge. Majukumu yanatuita tuyatumize. Ninapenda kuwa mwanaume.

Iwapo wewe ni mwanamume, inakupasa upende kuwa mwanamume. Zaidi ya hapo, unahitaji kupenda uwe mwanamume wa kifalme. Kuwa mwanamume wa kifalme ni hatima ya kila mwanamume. Na kila mwanamke huwa na ndoto ya kuwa na mmoja kama huyo . Kwa sababu, mwanaume wa kifalme anapotawala eneo lake vyema, kila mmoja hufaidi.

Kila mmoja anaweza kupumzika vyema.

Katika nyumba ya Evans, tunayo ishara tatizo linapotokea. Ni vidole vitatu. Ni hayo tu. Ninapoinua vidole vitatu, na bila ya kusema neno, mara moja naona hali ya wasiwasi kwenye uso wa mke wangu au kwa yeyote ninayezungumza naye aondoke. Huondoka kwa sababu vidole hivyo vitatu vyawakumbusha kwamba: Nimeelewa.

Nimeelewa.

Nisemapo, “Nimeelewa,” ina maana kwamba, yule ninayezungumza naye hana haja ya kulibeba jambo hilo, kuwa na wasiwasi kulihusu au kujaribu kutatua. Naliwajibikia. Na ikiwa ni jambo nisiloweza kulitatua, nitatoa faraja, uthabiti, na huruma inayohitajika ili kupitia wakati huo.

Haina maana utafanya kila kitu katika uhalisi na udhahiri wake. Ina maana kwamba utahakikisha kuwa kila kitu kimefanyika.

Unapokuwa umewadhihirishia kwa walio ndani ya eneo lako la ushawishi kwamba unaweza kutegemewa, unawajibika, na kwamba unawajibika urekerekebishaji, kusuluhisha au kwa urahisi kuubebea mzigo ambao haungeliweza kutatuliwa, basi utakuwa umewaweka huru kupumzika. Umewaweka huru wapumzike kwa sababu wanajua kwamba wanaweza kumwamini mwanaume ambaye amewathibitishia kwa vitendo vya zamani kwamba, anaelewa. Kama mwanamume wa kifalme, wale wanaokuzunguka wanahitaji kujua kwamba unaelewa.

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Kusaka Ukuu

Wanaume hutamani kuwa wakuu. Sio tu kwamba tunatamani kuwa wakuu, bali pia tunatamani kutambuliwa kuwa wakuu. Lakini wanaume wengi hutatatizika wanapotaka kunufaika na uwezo wao wa kweli nao huishia kukimbizana na mambo yanayowapeleka mbali zaidi na pale wanapotaka kuwa. Gundua uanaume halisi na Tony Evans.

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/