Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kusaka UkuuMfano

Kusaka Ukuu

SIKU 6 YA 7

Mwanamume wa Kifalme

Ajenda ya Mungu ni kuendeleza ufalme wake katika kila eneo la maisha na ili afanye hivyo, anatafuta wanaume watakaojitokeza katika jitihada zao kwa ukuu. Hata hivyo ili kupanda kwenye hafla hiyo ya ukuu, ni lazima kwanza ujiruhusu, ujiachilie - ujipe ruhusa - na kuitaka. Uliumbwa kwa ajili yake. Ni sawa kuitaka. Kwa kweli ni zaidi ya sawa – ni agizo.

Wanaume wengi sana wameridhika na kikosi cha mazoezi. Wanaume wengi sana wanaridhika na kuwa sawa tu, kuvumilia, au kuishi maisha yasiyosisimua na ya kawaida. Nyingi, ikiwa si hivyo basi baadhi, ya matatizo tunayokumbana nayo leo ni kwa kuwa mawazoa ya wanaume ni ndogo mno. Aidha wao hawafikirii juu ya ukuu hata kidogo, au wanafikiria vibaya kulingana na mtazamo wa kiulimwengu kuhusu ukuu.

Wezi fulani siku moja walivunja na kuingia kwenye duka, ila hawakuiba chochote. Walibadilisha vibandiko vya bei tu. Walichukua kibandiko cha $12,000 iliyokuwa kwenye saa ya Rolex na kukibandika kwenye ile ya Timex. Wakachukua kibandiko cha $99 kilichokuwa kwenye saa ya Timex na kukiweka kwenye saa ya Rolex. Walifanya hivyo kwa kila kitu kilichokuwa kwenye duka lile. Siku iliyofuatia watu waliingia kwenye duka na kununua mafungu la bidhaa, walitumia pesa nyingi kwa visivyokuwa na thamani na pesa kidogo kwa vilivyokuwa ghali.

Twaishi katika tamaduni leo hii, yenye vibandiko vilivyo badilishwa kuhusu ukuu. Imeweka pesa nyingi kwa maisha ya raha, na kubandika thamani ya $99 kwa tabia. Imeweka pesa nyingi sana kwenye magari na kazi, lakini senti kumi tu kwenye unyofu, familia na ushawishi.

Mungu anasimama kwenye chumba cha kubadilishia cha nafsi zetu akiwa na zabuni ya kibinafsi kwa ukuu, mradi, ukuu huo uwe chini ya mamlaka yake, na kudhihirika kwake kuwe katika bidii ya kuakishi utukufu wake. Jambo ambalo ulimwengu kikawaida haisemi kuwa ni lenye thamani, lakini ni kitu ambacho umilele imeona kuwa yenye thamani kubwa.Kuelewa thamani ya ukuu wa kweli ni ufunguo ya kuwa na uzoefu wa yote uliyohitimishwa kuwa.

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Kusaka Ukuu

Wanaume hutamani kuwa wakuu. Sio tu kwamba tunatamani kuwa wakuu, bali pia tunatamani kutambuliwa kuwa wakuu. Lakini wanaume wengi hutatatizika wanapotaka kunufaika na uwezo wao wa kweli nao huishia kukimbizana na mambo yanayowapeleka mbali zaidi na pale wanapotaka kuwa. Gundua uanaume halisi na Tony Evans.

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/