Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kusaka UkuuMfano

Kusaka Ukuu

SIKU 7 YA 7

Mwanamume wa Kifalme

Mwezi hauna mwanga wake. Kile tuonacho tunaposhuhudia ukuu wa mwezi usiku watokana na akisi ya mwangaza utokao kwa jua. Japo Mungu alikuumba uwe mkuu, ukuu wako ni lazima siku zote iwe ni akisi yake mwenyewe. Ukuu wa Mungu, ambao unafaa kuakisi, ilidhihirishwa kwa uwazi kwa Mwana wake, ambaye, “hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi” (Mathayo 20:28).Kwa maneno mengine, ukuu wako ni lazima uwafanye wengine walioko katika eneo lako la ushawishi kuwa bora, na siyo kudorora.

Ukuu wako wafaa kuwatia motisha wanaume wengine watake kuwa kama wewe, kwa sababu wanaona athari kwa wema katika maisha ya wengine.

Kufikia ukuu haina maana kwamba jina lako litakuwa katika mianga ya ubao unao onyesha mabao. Kufikia ukuu ina maana ya kutumikisha uwezo wako wote katika hatima yako, kwa utukufu wa Mungu na kwa wema wa wengine. Kati ya wachezaji wakuu katika timu ya soka ya kimerikani ni mpimaji. Kati ya wachezaji wakuu katika timu ya soka ya kimerikani ni mpimaji. Ikiwa mpimaji huyo hatapiga mpira kila mara kwa timu pinzani kusudi awachanganye zaidi uwanjani, mchezo waweza kubadilika. Kasi ya mchezo inaweza kubadilika. Mabao yanaweza kubadilika. Matokeo yanaweza kubadilika.

Je! Hata ni mashabiki wangapi wanaoweza kujua jina la mpimaji katika timu hizo za soka?

Lakini, iwe anajulikana au hajulikani, yamhitaji awe mkuu.

Ujulikane au usijulikane, ni lazima uwe mkuu.

Ukuu kwa mwanamume wa kifalme huanza kwa kujiweka chini ya ajenda ya ufalme wa Mungu, na kwa kufanya hivyo kuwanufaisha wengine. Fanya uamuzi kwamba, sio tu kwamba unataka ukuu, lakini utaenda kuufuata kulingana na njia ya Mungu ya kuupata. Sasa, ninaelewa kwamba kufanya uamuzi huo kunaweza kuwa mgumu. Labda unajihisi kana kwamba hali ya maisha haijawa ya kukutendea haki. Yaweza kuwa sababu tofauti kwa wanaume tofauti.Pengine unakabiliwa na ubaguzi wa rangi, au labda ulilelewa bila baba au mfano mzuri wa kiume Huenda waishi katika shimo la kifedha, au pengine wafanya kazi wenzio, au mkuu wako kazini hawakutendi haki. Huenda ni familia ambayo ina vurumai au tayari umeweka mwelekeo wa uongozi wako ni ule wa kimya kimya katika nyumba yako.

Haijalishi uwezekano wa kushindwa kwako, usiruhusu huo uamue hatima yako. Mungu amekupangia ukuu kuwa hatima yako. Yesu alisema, ikiwa utamwamini, utayatenda mambo makuu kuliko aliyotenda. Hakusema kwamba inawezekana uyatende. Wala hakusema kama waweza kuyatenda. Yesu alisema, ukiamini, utayatenda.

Utayayatenda.

Tunatumahi kuwa mpango huu ulikuhimiza. Kwa habari zaidi kuhusu wizara, bofya hapa.

siku 6

Kuhusu Mpango huu

Kusaka Ukuu

Wanaume hutamani kuwa wakuu. Sio tu kwamba tunatamani kuwa wakuu, bali pia tunatamani kutambuliwa kuwa wakuu. Lakini wanaume wengi hutatatizika wanapotaka kunufaika na uwezo wao wa kweli nao huishia kukimbizana na mambo yanayowapeleka mbali zaidi na pale wanapotaka kuwa. Gundua uanaume halisi na Tony Evans.

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/