Kusaka UkuuMfano
Mwanamume wa Kifalme
Swali lilo sakafuni tunapoanza mwendo wa kuingia katika eneo hili la kufanyika kuwa mwanamume wa kifalme ni hili – kwanza kabisa, tulifikaje mahali hapa? Ni kwa jinsi gani sisi - taifa lenye msingi wake ulioko katika kanuni za jumuiya na uwajibikaji wa binafsi wa kiroho – tumeishia kuzama katika bahari ya wanaume wengi wasiowajibika? Jibu la swali hilo si gumu kama vile waweza kuwaza. Kwa kweli yote haya yanahusiana na Kitabu cha Ufalme. Mahali fulani katika mwendo, tumesahau kushauriana na Kitabu tulichopewa ambacho kwayo tutawale.
Hatuwezi kutarajia kuelewa au kuishi kulingana na ufafanuzi wa Mungu kuhusu uanaume halisia pasipo kutumikisha maudhui yaliyomo kwenye neno lake. Ofisa anayefanya urefa akisimamia mchezo kwa kutumia sehemu ya kitabu cha masharti, yuaweza kuachishwa kazi mara moja.Hadi sasa, kwa sababu fulani, sisi kama wanaume tumeshindwa kutambua kwamba ni lazima kuishi maisha yetu yote kwa Neno hilo kamili la Mungu. Wakati wowote Neno la Mungu linapotoshwa, kuwekewa mipaka au utawala wake mkuu kupunguzwa katika maisha ya mwanamume, basi majeruhi watakuwepo. Kama vile wanafanya leo. Na kama vile ilivyokuwa katika bustani miaka maelfu iliyopita. Kama walivyofanya na Adamu.
Mjadala wowote kuhusu jukumu, kusudi na uongozi wa mwanamume lazima uanze kwa Adamu. Theolojia ya Adamu si dhana tu ya maneno matupu yaliyoko katika Agano la Kale. Ni theolojia ya uwajibikaji wa mwanamume kulingana na taratibu ya uumbaji, na kile ambacho Mungu alimwajibisha kwalo yaonekana katika Agano Jipya na hata katika wakati wa kanisa.
Sababu iyo hiyo ya sisi kutoweza kupata watu wanaosimamia kazi zao leo ni sababu iyo hiyo Mungu alipitia bustani zamani sana akisema, "Adamu, uko wapi?"
Kilichosababisha Adamu asipatikane bustanini siku hiyo ndicho hicho hicho kinachosababisha wanawake vijana wengi kuwa na ugumu wa kumpata Adamu siku hizi. Na sababu iyo hiyo, ndiyo imewafanya wanawake wengi waliooolewa wanakatishwa tamaa na Adamu ambaye wamempata. Hii pia ni sababu sawa kwa nini wachungaji na viongozi wa makanisa wanaona ni vigumu kuwaweka wanaume kulinda kwenye kazi zao.
Sababu hii ni kwamba wanaume wamekosa kuelewa jukumu lao la kuongoza kama mwanamume wa kifalme.
Kuhusu Mpango huu
Wanaume hutamani kuwa wakuu. Sio tu kwamba tunatamani kuwa wakuu, bali pia tunatamani kutambuliwa kuwa wakuu. Lakini wanaume wengi hutatatizika wanapotaka kunufaika na uwezo wao wa kweli nao huishia kukimbizana na mambo yanayowapeleka mbali zaidi na pale wanapotaka kuwa. Gundua uanaume halisi na Tony Evans.
More
Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/