Bibilia Ya WatotoMfano
MUNGU ALIUMBA VITU VYOTE! Wakati Mungu alimuumba mtu wa kwanza, Adamu, aliishi katika bustani la Edeni na bibi yake Hawa. Waliishi kwa raha wakimtii Mungu na kufurahia uwepo wake hadi siku moja . . .
“Mungu aliwaamri msile matunda ya miti yote, sivyo?” nyoka akamwuliza Hawa. “Tunaweza kula matunda ya miti yote ila moja,” Hawa akajibu. “Tukila tunda la hilo mti, tutakufa.” “Hamtakufa,” nyoka akamdanganya. “Mtakuwa kama Mungu.” Sasa Hawa akatamani tunda la huo mti aliokatazwa na Mungu. Alimsikiza nyoka na akala tunda lile.
Baada ya Hawa kutomtii Mungu, alimuongoza Adamu naye pia akala lile tunda. Adamu alitakikana kumueleza Hawa, “La! Sitakubali kutotii neno la Mungu.”
Baada ya Adamu na Hawa kutenda dhambi, walikuja kugundua kuwa walikuwa uchi. Kwa hivyo, wakashona matawi ya miti kuwa mavazi na kujificha ndani ya misitu kutokana na uwepo wa Mungu.
Katika barizi ya jioni, Mungu akaja shambani. Alijua kuwa Adamu na hawa walikuwa wametenda dhambi. Adamu alimlaumu Hawa. Hawa alimlaumu nyoka. Mungu akasema, “Nyoka amelaaniwa. Mwanamke pia atapitia machungu anapozaa watoto.”
“Adamu, Kwa vile umetenda dhambi, ardhi imelaaniwa na miiba. Binadamu atalima na kutoa jasho ndipo apate chakula.”
Mungu akawatoa Adamu na hawa nje ya bustani lile zuri. Kwasababu walitenda dhambi, walitenganishwa na Mungu mwenye uhai!
Mungu akatengeneza upanga wa moto wa kutunza Bustani la Edeni. Pia Mungu akawatengenezea Adamu na Hawa mavazi kutokana na ngozi. Mungu alitoa ngozi wapi?
Kwa wakati, familia ikazaliwa kwa Adamu na Hawa. Mwana wao wa kwanza Kaini, alikuwa mkulima. Mwana wao wa pili, Habili, alikuwa mchungaji wa wanyama. Siku moja Kaini alimletea Mungu mimea ya shamba kama sadaka. Habili akamletea kondoo wake mzuri zaidi ya wote kama sadaka. Mungu alifurahia sadaka ya Habili.
Mungu hakufurahia sadaka ya kaini. Kwa hivyo Kaini akawa na hasira. Lakini Mungu akasema, “Ukitenda kile kilicho sawa utakubaliwa, sivyo?”
Hasira ya Kaini ikazidi kumpanda. Baada ya wakati usio mrefu alimvamia nduguye Habili – na akamwua!
Mungu akamzungumzia Kaini. “Yuko wapi ndugu yako Habili?” “Sijui,” Kaini akadanganya. “Mimi ni mwekaji ndugu yangu?” Mungu akamwadhibu Kaini kwa kumnyang’anya uwezo wake wa ukulima na kumfanya awe mtu anayezurura ovyo.
Kaini aliondoka kutoka uwepo wa Mwenyezi Mungu. Akamwoa binti wa Adamu na Hawa. Hapo wakakuza jamii. Katika wakati usio mrefu, wajukuu na vitukuu wa Kaini wakajaza mji ambao aliuanzisha.
Wakati huo huo, familia ya Adamu na Hawa ikazidi kuongezeka. Wakati mwana wake Sethi alizaliwa, Hawa akasema, “Mungu amenipa Sethi kwa nafasi ya Habili.” Sethi alikuwa mcha Mungu aliyeishi miaka 912 na akawa na watoto wengi.
Duniani, watu walizidi kuwa waovu vizazi vilivyoendelea kuongezeka. Mwishowe, Mungu akaamua kuwaangamiza wanadamu na wanyama wote na ndege. Mungu alijuta kumwumba binadamu. Lakini mtu mmoja alimpendeza Mungu . . .
Mtu huyu alikuwa Nuhu. Alikuwa wa jamii ya sethi, Nuhu alikuwa mtakatifu na asiye dhambi. Alitembea naye Mungu. Pia aliwafunza wana wake watatu jinsi ya kumtii Mungu. Sasa, Mungu akapanga kumtumia Nuhu kwa njia ya ajabu na kipekee!
Mwisho
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Je! Yote ilianzaje? Tulikuja wapi? Kwa nini kuna mateso mengi duniani? Je! Kuna tumaini? Je! Kuna uzima baada ya kifo? Pata majibu unaposoma historia hii ya kweli ya ulimwengu.
More
Tungependa kuwashukuru Bible for Children, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://bibleforchildren.org/languages/swahili/stories.php