Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Bibilia Ya WatotoMfano

Bibilia Ya Watoto

SIKU 4 YA 7

Hapo zamani, Mungu alimtuma malaika Gabrieli kwa mwanamali mdogo n a wa kupendeza aliyeitwa Maria. Akamwambia, “Wewe utazaa mwana na jina lake utamuita Yesu. Yeye ataitwa mwana wa aliye juu. Yeye atamiliki milele.”

“Hii itakuaje?” binti Yule aliuliza akiwa ameshangaa. “Mimi sijaolewa na mwanamume yeyote.” Malaika akamwambia Maria kuwa mtoto angetoka kwa Mungu. Mtoto Yule hangekuwa na baba wa kibinadamu.

Malaika pia akamwelezea Maria kuwa jamaa yake Elisabeti alikuwa amepata mimba katika uzee wake.

Maria alikuwa amepanga kuolewa na Yusufu. Yusufu alisikia vibaya aliposikia kuwa Maria alikuwa mjamzito. Alidhania kuwa mwanamume mwingine alikuwa ndiye baba ya mtoto.

Katika ndoto, malaika wa Mungu alimwambia Yusufu ya kuwa huyu alikuwa mwana wa Mungu. Naye Yusufu alikuwa amsaidie Maria kumlelea Yesu.

Yusufu alimwamini na kumtii Mungu. Naye pia alitii amri za nchi yake. Kwasababu ya amri moja, Yusufu na Maria walisafiri kutoka kwao hadi Bethlehemu, ili kulipa ushuru.

Maria alikuwa tayari kumzaa mtoto. Lakini Yusufu hakuweza kupata nyumba ya kukaa. Nyumba zote zilikuwa zimejaa.

Mwishowe Yusufu aliweza kupata malazi horini. Hapo, mtoto Yesu akazaliwa. Mama yake akamlaza ndani ya hori la kulia la ng’ombe.

Karibu na hapo, wachungaji walikuwa wakiwachunga kondoo wao. Malaika wa Mungu akawatokea na kuwapa habari lile njema. “Amezaliwa kwenu siku ya leo katika mji wa Daudi mwokozi, ndiye Kristo Bwana. Mtamkuta mtoto amelala katika hori ya kulia ya ng’ombe.”

Ghafla, malaika wengi wengine wanaong’aa wakatokea, wakimsifu Mungu wakisema, “Atukuzwe Mungu juu mbinguni, na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia.”

Wachungaji wakaharakisha kuelekea horini. Baada ya kumwona mtoto walimweleza kila waliokutana nao kumhusu Yesu.

Muda wa siku arobaini baadaye, Yusufu na Maria walimleta Yesu kwenye hekalu kule Yerusalemu. Hapo, mwanamume aliyeitwa Simioni alimtukuza Mungu kwa sababu ya mtoto, naye Anna, mtumishi mwingine wa Mungu, akamshukuru Mungu. Wote walifahamu kuwa Yesu alikuwa mwana wa Mungu, mwokozi aliyekuwa ameahidiwa. Yusufu akawatoa ndege wawili kama sadaka. Hii ilikuwa sadaka ambayo kulingana na amri ya Mungu watu masikini walipaswa kuleta walipokuwa wanamletea Mungu mtoto aliyezaliwa.

Muda mfupi ulipopita, nyota ya kipekee iliwaongoza wazee watatu wenye hekima kutoka nchi ya Magharibi kuja Yerusalemu. “Yuko wapi Mfalme wa Wayahudi aliyezaliwa?” wakauliza. “Tunataka kumwuabudu.”

Mfalme Herodi akasikia kuwahusu wale wazee wenye hekima. Akiwa na wasiwasi akawaambia wamueleze watakapompata Yesu. “Pia nami nataka kumwuabudu.” Herodi akawaambia. Lakini alikuwa anawadanganya. Herodi alitaka kumwua Yesu.

Ile nyota ikawaongoza hadi horini Maria na Yusufu walimokaa na mtoto Yesu. Wakipiga magoti wakimwuabudu, wale wasafiri walimpa Yesu zawadi za kupendeza za dhahabu na manukato.

Mungu akawapa wale wazee hadhari kuwa warudi nyumbani kisiri. Herodi alikasirika sana alipogundua haya. Kwa hamu ya kumwuangamiza Yesu, kiongozi huyu mwovu aliwaua watoto wote wachanga wa kiume kule Bethlehemu.

Lakini Herodi hangeweza kumwangamiza mwana wa Mungu! Walipohadhariwa kwa ndoto, Yusufu aliwachukua Maria na Yesu penye usalama kule Misri.

Herodi alipoaga dunia, Yusufu akawatoa Maria na Yesu Misri. Wakaishi katika mji mdogo wa Nazareti iliyokuwa karibu na ziwa la Galili.

Mwisho

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Bibilia Ya Watoto

Je! Yote ilianzaje? Tulikuja wapi? Kwa nini kuna mateso mengi duniani? Je! Kuna tumaini? Je! Kuna uzima baada ya kifo? Pata majibu unaposoma historia hii ya kweli ya ulimwengu.

More

Tungependa kuwashukuru Bible for Children, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://bibleforchildren.org/languages/swahili/stories.php