Bibilia Ya WatotoMfano
Ni nani aliyetuumba? Bibilia, Neno la Mungu, linatueleza jinzi viumbe vyote alivyoanza. Hapo mwanzo Mungu aliumba mwanadamu wa kwanza akamuita Adamu. Mungu alimuumba Adamu kutoka kwa mavumbi ya ardhi. Mungu alipopuliza uhai ndani ya Adamu, alikuwa hai. Akijipata katika bustani maridadi ya Edeni.
Kabla Mungu kumuumba Adamu, aliumba ulimwengu maridadi uliojazwe na vitu vya kustaajabisha. Hatua baada ya nyingine Mungu alifanya vilima na anga, maua ya manukato mazuri, na miti mirefu, ndege wa angani na nyuki, samaki wa majini na konokono. Ama kweli, Mungu ndiye aliyeumba vyote vionekanavyo.
Hapo mwanzo, kabla Mungu kuumba chochote, hakukuwa na chochote ila Mungu. Hapakuwa na watu ama, mahala popote au vitu vyovyote. La. Hapana mwanga wala giza. Hapakuwa na milima wala mabonde. Jana na kesho hazikuwepo. Palikuwa tu Mungu asiyekuwa na mwanzo. Mungu akajukuwa hatua.
Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi.
Na nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu. Na giza ilikuwa juu ya vilindi vya maji. Kishi Mungu akasema, “Iwe nuru”.
Pakawa nuru. Mungu akaita nuru Mchana na giza akaita Usiku. Jioni na asubuhi hiyo ikawa siku ya kwanza.
Kwenye siku ya pili, Mungu akayaweka maji ya bahari, ziwa na mito kwa mpangilio chini ya mbingu. Siku ya tatu, Mungu akasema, maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, ili pakavu paonekane; ikawa hivyo.
Mungu akaiamuru nchi kutoa majani, mche utoao mbegu, na mti wa matunda uzaao matunda kwa jinsi yake ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo. Ikawa jioni, ikiwa asubuhi, siku ya tatu.
Mungu akafanya jua, mwezi na nyota nyingi zisizohesabika. Ikawa jino na asubuhi siku ya nne.
Viumbe vya bahari, samaki na ndege ndivyo vilivyo fuatilia kwa orodha ya Mungu. Siku ya tano Mungu akaumba nyangumi wakubwa na akila kiumbe chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa jinsi zao, na kila ndege arukaye, kwa jinsi yake; ikawa jioni, ikawa asubuhi siku ya tano.
Baada ya hayo, Mungu akanena tena, akasema, “Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwito kwa jinsi zake; ikawa hivyo.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi siku ya sita.
Mungu alifanya kitu kingine tofauti kwa siku ya sita - kitu cha maana sana. Vitu vyote vilikuwa tayari kwa mwanadamu. Viakula vilikuwa mashambani na wanyama wa kumtumikia, Mungu akasema, “Natufanye mtu kwa mfano wetu. Na awe mtawala wa vitu vyote nchini.” BASI MUNGU AKAUMBA MTU KWA MFANO WAKE; KWA MFANO WA MUNGU ALIMUUMBA ...
Mungu akanena na Adamu. “Kula chochote utakacho kutoka kwenye bustani. Lakini usile kutoka kwenye mti wa ujuzi wa kujua mema na mabaya. Mkila kutoka kwa mti huo hakika mtakufa.”
Bwana Mungu akasema, “Si vyema huyo mtu awe peke yake, nitamfanya msaidizi wa kufanana naye.” Bwana Mungu akafanyiza kutoka katika ardhi kila mnyama wa msituni, na kila ndege wa angani, akamletea Adamu ili aone atawaitaje; kila kiumbe hai, jina alilokiita Adamu likawa ndili jina lake. Adamu akawapa majina wote. Alikuwa mwerevu sana kwa kutenda haya. Lakini hakuonekana wa kumsaidia Adamu aliyefanana naye.
Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, Mungu akafanya mwanamke kutoka kwa ubavu huo. Mwanamke huyu aliyeumbwa na Mungu alikuwa msaidizi wa kufanana na Adamu.
Kwa siku sita Mungu aliumba vitu vyote. Mungu akaibariki siku ya saba na kuiweka siku ya mapumziko. Katika bustani la Edeni, Adamu na mkewe Hawa walikuwa na furaha kamilifu kumutii Mungu. Mungu alikuwa Bwana wao, msaidizi na rafiki wao.
Mwisho
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Je! Yote ilianzaje? Tulikuja wapi? Kwa nini kuna mateso mengi duniani? Je! Kuna tumaini? Je! Kuna uzima baada ya kifo? Pata majibu unaposoma historia hii ya kweli ya ulimwengu.
More
Tungependa kuwashukuru Bible for Children, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://bibleforchildren.org/languages/swahili/stories.php