Bibilia Ya WatotoMfano
Hii hadithi ya bibilia inatueleza kumhusu Mungu wetu wa ajabu aliyetuumba na anayetaka tumjue.
Mungu anajua tumetenda mambo mabaya, anayoyaita dhambi. Adhabu ya dhambi ni mauti, lakini Mungu anakupenda sana hata akamtuma mwana wake wa pekee, Yesu, Ili afe msalabani na aadhibiwe kwa dhambi yako. Alafu Yesu akafufuka na kuenda nyumbani mbinguni! Ukimwamini Yesu na kumwomba msamaha kwa dhambi yako, Atakusamehe! Yesu atkuja na kuishi ndani yako, na utaishi naye milele.
Kama unaamini huu ni ukweli, Sema haya kwa Mungu: Mpendwa Yesu, ninaamini kuwa wewe ni Mungu, na ulifanyika mtu ili ufe kwa ajili ya dhambi zangu, ili niwe na maisha mapya, na siku moja nitaenda kuwa nawe millele. Nisaidie nikutii na niishi kwa ajili yako kama mtoto wako. Amina.
Soma bibilia na uzungumze na Mungu kila siku!
Kuhusu Mpango huu
Je! Yote ilianzaje? Tulikuja wapi? Kwa nini kuna mateso mengi duniani? Je! Kuna tumaini? Je! Kuna uzima baada ya kifo? Pata majibu unaposoma historia hii ya kweli ya ulimwengu.
More
Tungependa kuwashukuru Bible for Children, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://bibleforchildren.org/languages/swahili/stories.php