Bibilia Ya WatotoMfano
Mwanamke alisimama chini ya mlima palipokuwa na makelele, macho yake yenye huzuni yakitazamia ambapo palikuwa na jambo la kuhuzunisha. Mwana wake alikuwa anakufa. Mwanamke huyu alikuwa Maria, na alisimama mahali ambapo Yesu alikuwa amesulubishwa msalabani.
Haya yote yalitendekaje? Maisha ya Yesu ya kupendeza yangeishaje katika njia hii ya kutisha? Mungu alikubalia aje mwana wake asulubishwe msalabani hadi afe pale? Yesu alifanya kosa kuhusu yeye ni nani? Kweli Mungu alikosea pale?
La! Mungu hakukosea. Yesu hakuwa amefanya kosa lolote. Yesu alikuwa anajua kuwa atauliwa na watu waovu. Hata Yesu alipokuwa mtoto mchanga, mzee mmoja aitwaye Simioni alimwambia Maria kuwa wangepatwa na huzuni hapo mbele.
Siku chache kabla Yesu auawe, mwanamke mmoja alikuja na kumwaga manukato miguuni mwa Yesu. “Huyu anapoteza pesa bure,” wanafunzi wa Yesu walilalamika. “Ametenda jambo njema,” Yesu akasema. “Amelitenda kwa kuzikwa kwangu. Maneno ya kutisha haya!
Baada ya haya, Yuda Iskariote, mwanafunzi mmojakati ya kumi na wawili wa Yesu, alikubali kumsaliti Yesu kwa kuhani mkuu ili apate fedha 30.
Katika sikukuu ya wayahudi ya pasaka, Yesu alikula chakula chake cha mwisho pamoja na wanafunzi wake. Aliwaelezea maneno makuu kumhusu Mungu na ahadi zake kwa wale wanaompen- da. Halafu Yesu akawapa mkate na kikombe wagawane. Haya yalikuwa ya kuwakumbusha kuwa mwili na damu ya Yesu tulipewa ili kuleta msamaha wa dhambi.
Hapo Yesu akawaambia marafiki wake kuwa atasalitiwa na wao watatoroka. “Mimi sitatoroka,” Petero akasema. “Kabla jogoo hajawika leo, utanikana mara tatu,” Yesu akasema.
Baadaye usiku huo, Yesu alikwenda kuomba katika bustani Gethsemani. Wanafunzi wake waliokuwa naye wakasinzia. “Ee Baba,” Yesu aliomba, “... uniondolee kikombe hiki. Walakini si mapenzi yangu bali yako itendeke.”
Muda si muda kikundi cha watu wakaingia bustani mle, wakiwa wanaongozwa na Yuda. Yesu hakukataa, lakini Petro akakata sikio la mtu. Kimya, Yesu akamgusa sikio na kumponya. Yesu alijua kukamatwa kwake kulikuwa ni mapenzi ya Mungu.
Kikundi kile kilimchukua Yesu kwenye nyumba la kuhani mkuu. Pale, viongozi wa wayahudi wakasema kuwa Yesu lazima afe. Hapo karibu, Petero alikuwa anasimama karibu na moto la wafanyakazi akitazama. Mara tatu watu walimtazama Petero na kusema, “Wewe ulikuwa na Yesu!” Mara tatu Petero alikana, kama vile Yesu alisema atafanya. Petero hata alitukana.
Hapo, jogoo akawika. Ilikuwa ni kama sauti ya Mungu kwa Petero. Akikumbuka maneno ya Yesu, Petero akalia kwa majonzi.
Yuda alisikia vibaya pia. Alijua kuwa Yesu hakuwa ametenda chochote kibaya. Yuda alirudisha fedha ile thelathini lakini makuhani walikataa kuichukua. Yuda alitupa fedha ile chini, akaenda nje na kujinyonga.
Makuhani wakamleta Yesu mbele ya Pilato, mkubwa wa Warumi. Pilato akasema, “Sijapata kosa lolote na mtu huyu.” Lakini watu wakazidi kusema, “Asulubishwe! Asulubishwe!”
Mwishowe Pilato akakubali na kumhukumu Yesu kifo msalabani. Askari walimpiga Yesu na kumtemea mate usoni, na kumcharaza viboko. Walimtengenezea taji la miiba na kumvisha kichwani. Halafu wakamsulubisha msalabani kwa misumari ili afe.
Yesu alikuwa amejua tayari kuwa angekufa vile. Alijua pia kuwa kifo chake kingeleta msamaha wa dhambi kwa wale wamwaminio. Wahalifu wawili walisulubishwa kando yake. Mmoja alimwamini Yesu – na alienda paradiso. Yule mwingine hakumwamini.
Baada ya masaa ya kuteseka, Yesu akasema, “Imekwisha” na akafa. Kazi yake ilikuwa imeisha. Marafiki wake walimzika katika kaburi lililochongwa mwambani.
Halafu askari wa Warumi wakafunga na kulichunga kaburi. Sasa hakuna ambaye angeingia wala kutoka pale.
Kama hii ingekuwa mwisho wa hadithi, ingekuwa ya kuhuzunisha. Lakini Mungu akatenda jambo la ajabu. Yesu hakubaki kifoni!
Asubuhi na mapema ya siku ya kwanza katika wiki, wanafunzi wachache wa Yesu walipata jiwe limeondolewa kaburini. Walipoangalia ndani, Yesu hakuwa pale.
Mwanamke mmoja akabakia akilia. Yesu alimtokezea! Alikimbia na kuenda kuwaelezea wengine kwa FURAHA. “YESU YU HAI! YESU AMEFUFUKA KIFONI!”
Punde Yesu akaja walipokuwa wanafunzi wake na kuwaonyesha alama mikononi ya msumari. Ilikuwa kweli. YESU ALIKUWA HAI TENA! Alimsamehe Petero kwa kumkana, na akawaambia wanafunzi wawaeleze kila mtu kumhusu yeye. Halafu akarudi mbinguni alipotoka hiyo siku ya krismasi ya kwanza.
Mwisho
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Je! Yote ilianzaje? Tulikuja wapi? Kwa nini kuna mateso mengi duniani? Je! Kuna tumaini? Je! Kuna uzima baada ya kifo? Pata majibu unaposoma historia hii ya kweli ya ulimwengu.
More
Tungependa kuwashukuru Bible for Children, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://bibleforchildren.org/languages/swahili/stories.php