Bibilia Ya WatotoMfano
Nuhu alikuwa mwabudu Mungu. Watu wote wengine walimchukia na kutomtii Mungu. Siku moja, Mungu alisema jambo la kushtua. “Nitaiangamiza dunia hii iliyoharibika,” Mungu akamwambia Nuhu. “Wewe na jamii yako ndiyo mtakaookoka.”
Mungu alimpa ilani Nuhu kuwa mafuriko makuu yatatokea na kufunika ardhi yote. “Jenga safina,” machela kubwa inayotosha familia yake na wanyama wengi. Nuhu aliamrishwa. Mungu alimwuelezea kila atakacho fanya. Sasa Nuhu akaanza kazi!
Watu walimchekelea Nuhu alipojaribu kuwaelezea sababu yake ya kujenga safina. Hata hivyo, Nuhu aliendelea kujenga. Pia alizidi kuwaelezea kumhusu mungu. Hakuna aliyemsikiliza.
Nuhu alikuwa na imani kubwa. Almwuamini Mungu hata kama mvua haikuwa imewahi kunyesha hapo mbeleni. Baadaye safina ilikuwa tayari.
Sasa, wanyama wakaja. Mungu aliwaleta aina saba ya wanyama na wawili wa wengine. Ndege wakubwa kwa wadogo, wanyama warefu kwa wafupi wakaingia ndani ya safina.
Pengine watu walimtukana Nuhu alipokuwa akiwaingiza wanyama. Waliendelea kutenda dhambi. Hawakutaka kuingia ndani ya safina.
Mwishowe, wanyama wote na ndege wakawa ndani. “Njoo ndani ya safina,” Mungu akamualika Nuhu. “Wewe na familia yako.” Nuhu, bibi yake, wana wake watatu na bibi zao wakaingia ndani ya safina. Hapo Mungu akaufunga mlango wa safina!
Mvua mkubwa ukaanza kunyesha. Kulinyesha kwa muda wa siku arobaini.
Maji yalifurika na kufunika miji na vijiji. Wakati mvua uliisha, hata milima ilikuwa imefunikwa. Kila kitu chenye uhai kilikufa.
Mafuriko yalipozidi nayo safina iliendelea kuelea juu ya maji. Labda kulikuwa na giza ndani, labda hakukuwa na starehe au hata kulikuwa kunatisha ndani ya safina. Lakini safina iliwapa Nuhu na jamii yake usalama.
Baada ya miezi mitano ya mafuriko, Mungu alituma upepo wa kukausha maji. Kwa muda, safina ikaja kutulia juu ya milima ya Ararat. Nuhu walikaa ndani ya safina kwa muda wa siku arobaini maji ilipozidi kupungua.
Nuhu akamtuma kunguru na njiwa nje ya safina kupitia dirisha. Alipokosa mahali pa kutua, njiwa akarudi.
Baada ya wiki, Nuhu akajaribu tena. Wakati huu njiwa alirudi na jani bichi la mzeituni kinywani mwake. Siku iliyofuata Nuhu akajua kuwa ardhi ilikuwa imekauka kwa vile njiwa hakumrudia.
Mungu akamwambia Nuhu kuwa wakati wa kutoka nje ya safina ulikuwa umefika. Pamoja, Nuhu na familia yake wakawasaidia wanyama kutoka.
Nuhu alijawa shukurani! Hapo, akatengeneza madhabahu ambapo walimwabudu Mungu ambaye aliwaokoa kutokana na mafuriko.
Mungu alimpa Nuhu ahadi ya ajabu. Kuwa hatawahi kutuma mafuriko kuja kumhukumu binadamu. Mungu akaweka kumbusho la ajabu la agano yake. Upinde ndio ulikuwa ishara ya ahadi hiyo.
Nuhu na familia yake wakapata mwanzo mpya baada ya mafuriko. Kwa wakati, vizazi vya Nuhu wakajaza ardhi mara nyingine. Mataifa yote ya dunia yalitoka kwa Nuhu na watoto wake.
Mwisho
Kuhusu Mpango huu
Je! Yote ilianzaje? Tulikuja wapi? Kwa nini kuna mateso mengi duniani? Je! Kuna tumaini? Je! Kuna uzima baada ya kifo? Pata majibu unaposoma historia hii ya kweli ya ulimwengu.
More
Tungependa kuwashukuru Bible for Children, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://bibleforchildren.org/languages/swahili/stories.php