Bibilia Ya WatotoMfano
Yesu alipokuwa akiishi duniani aliwaeleza wanafunzi wake kuhusu mbinguni. Alipaita “Nyumbani mwa Baba Yangu”, na akasema kuwa kule kuna makao mengi ya kupendeza. Mbinguni ni kubwa na kupendeza kuliko nyumba yoyote hapa duniani.
Yesu akasema, “Ninaenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu.” Yesu alienda mbinguni baada ya kufufuka kifoni. Wanafunzi wake wakitazama, Yesu alichukuliwa juu, na wingu likamchukua ili wasimwone tena.
Tangu hapo, wakristo hukumbuka ahadi ya Yesu kuwa atarudi kuwachukua. Yesu alisema kuwa atarudi ghafla, wakati ambao hawamtarajii. Lakini, je wakristo watakaokufa kabla hajaja? Bibilia inasema wataenda moja kwa moja kuwa na Yesu. Kutokuwa kwa mwili ni kuwa na Yesu.
Ufunuo, kitabu cha mwisho cha bibilia, inatueleza jinsi mbinguni ni ya ajabu. Kitu cha kushangaza ni kuwa, katika njia ya kipekee, mbinguni ni nyumbani mwa Mungu. Mungu yupo kila mahali lakini enzini kwake ni mbinguni.
Malaika na viumbe vingine mbinguni wanamwuabudu Mungu mbinguni. Pia watu wote wa Mungu waliokufa na kuenda mbinguni wanamwuabudu. Wanaimba nyimbo za sifa kwa Mungu.
Haya ni maneno kutoka wimbo moja wao huimba: WEWE UNASTAHILI KWA KUWA WEWE UMETUREJESHA KWA MUNGU KUPITIA DAMU YAKO KWA KILA KABILA NA TAIFA NA UMETUTENGENEZA WAFALME NA MAKUHANI KWA MUNGU WETU. (Ufunuo 5:9)
Kurasa za mwisho katika bibilia zinaelezea mbinguni kama “Yerusalemu Mpya”. Ni kubwa ajabu, ikiwa na kuta za juu nje. Kuta zimeundwa kwa yaspi, mfano wa kioo safi. Vito vya ajabu vimepamba kuta, ziking’aa na rangi za kupendeza. Kila mlango imeten-genezwa na lulu moja kubwa!
Hiyo milango ya lulu huwa wazi kila wakati. Tuingie ndani tukaone zaidi.. WAAA! Mbinguni ni ya kupendeza hata zaidi ndani. Mji ule ni wa dhahabu safi, kama kioo kiangavu. Hata njia ni ya dhahabu.
Mto wa maji safi ya uzima, wenye kung’aa unatirirka ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu. Upande huu na upande ule wa mto kuna mti wa uzima, ambao ulipatikana kwanza katika bustani ya Edeni. Mti huu ulikuwa wa kipekee. Ulikuwa unazaa matunda aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda aina tofauti kila mwezi. Na majani ya mti huo ni wa kuponya mataifa.
Mbinguni haiitaji jua wala mwezi kuangaza. Utukufu wa Mungu hutia nuru ya ajabu. Hakuna usiku kule hata kamwe.
Hata wanyama mbinguni ni wa aina tofauti. Wote ni watulivu na wenye urafiki. Mbwa mwitu na mwana kondoo wanakula nyasi pamoja. Hata simba wanakula nyasi kama ng’ombe. Bwana anasema, “Hawataumia wala kuangamia katika mlima wangu mtakatifu.”
Tunapozidi kutazama, tunagundua kuwa kuna vitu vinavyokosa mbinguni. Hakuna maneno ya hasira. Hakuna mtu anayepigana au kunyima. Hakuna vifunguo mlangoni kwa kuwa hakuna wezi mbinguni. Hakuna waongo, wauaji, wachawi au watu wengine waovu. Hakuna dhambi ya aina yoyote mbinguni.
Mbinguni kwa Mungu hakuna kilio tena. Wakati mwingine watu wa Mungu hulia kwasababu ya mateso makuu ya maisha haya. Mbinguni, Mungu atapanguza machozi yote.
Hakuna kifo mbinguni pia. Watu wa Mungu watakaa milele na Bwana. Hakutakuwa na mateso, kilio, uchungu tena. Hakutakuwa na magonjwa, kuachana, matanga tena. Kila mtu ataishi kwa furaha na mungu.
Kupendeza zaidi, mbinguni ni ya wasichana na wavulana (na watu wazima pia) ambao wamemwamini Yesu Kristo kama mwokozi na kumtii kama Bwana wao. Mbinguni kuna kitabu kiitwacho Kitabu cha Mwana kondoo cha Uzima. Kimejaa majina ya watu. Je, wajua ni majina ya nani yaliyo andikwa? Ni watu ambao wameweka tumaini yao kwa Yesu. Je, jina lako limo ndani?
Maneno ya mwisho ya bibilia ina ukaribisho wa ajabu. “Na Roho na Bibi-arusi wasema, ‘njoo!’ Naye mwenye kiu aje. Na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure.”
Mwisho
Kuhusu Mpango huu
Je! Yote ilianzaje? Tulikuja wapi? Kwa nini kuna mateso mengi duniani? Je! Kuna tumaini? Je! Kuna uzima baada ya kifo? Pata majibu unaposoma historia hii ya kweli ya ulimwengu.
More
Tungependa kuwashukuru Bible for Children, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://bibleforchildren.org/languages/swahili/stories.php