Kuishi kwa Roho: Ibada Pamoja na John PiperMfano
Roho ni Furaha ya Mungu
Roho Mtakatifu ni Mungu. Mtu akaaye ndani yetu, hutuongoza, na husafisha si mwingine zaidi ya Mungu, Roho Mtakatifu. Ushahidi rahisi wa hili ni cheo cha mara kwa mara " Roho wa Mungu." Roho ni "wa Mungu" siyo kwa sababu Mungu alimuumba, lakini kwa sababu anashiriki asili ya Mungu na milele anatoka kwa Mungu (angalia " Wakorintho 2:10-12)
Kama mwana wa Mungu milele ni sawa na Baba, kama Yohana 1: 1 inavyoweka wazi kwamba ndivyo alivyo, basi ndivyo na Roho Mtakatifu alivyo milele na wote, kwa sababu, kulingana na Warumi 8:9–11, Roho wa Kristo ni mmoja na sawa na Roho wa Mungu. Kama isingekuwa hivyo, tungeweza kufikiria kwamba kuna wakati Mwana hakuwa na Roho na Baba hakuwa na Roho. Lakini Roho Mtakatifu ni muhimu katika uhusiano kati ya Baba na Mwana. Ni, kwa kutumia maneno ya Handley C.G. Moule’s, “Matokeo, Kiungo, Chombo, cha furaha na upendo pamoja milele” (Mtu na Kazi ya Roho Mtakatifu, uk. 28).
Kutoka mbali katika umilele kama Mungu Baba alivyompenda Mwanawe, kumekuwa na furaha na upendo wa Roho Mtakatifu usioisha kati yao, ambaye yeye mwenyewe ni utu wa kiungu. Kwa hiyo, kama Yesu alivyoomba kwa ajili ya kanisa katika Yohana 17:26, hamuombi Baba chochote zaidi ya Roho Mtakatifu anaposema “Nami naliwajulisha jina lako, tena nitawajulisha hilo; ili pendo lile ulilonipenda mimi liwe ndani yao, nami niwe ndani yao.
Kweli ya utukufu kati ya kweli zote ambazo tutazivumbua katika masomo haya 7 ni kwamba Roho Mtakatifu anapokuja katika maisha yetu, haji tuu kama Roho wa Mwana, wala kama Roho wa Baba, lakini kama Roho wa upendo wa milele kati ya Baba na Mwana, ili tumpende Baba kwa upendo uleule wa Mwana, na kumpenda Mwana kwa upendo uleule wa Baba.
Jifunze zaidi: http://www.desiringgod.org/messages/the-holy-spirit-he-is-god
Kuhusu Mpango huu
Masomo 7 ya Ibada kutoka kwa John Piper kuhusu Roho Mtakatifu
More